Afrika Inuka 2023 | Siku ya 2 | Mlima wa Familia

TUME LINDA: Mtume alisema kwamba Mungu ni wa vizazi na kwamba mungu ndiye muanzilishaji wa familia, na Familia yote ambao haina msingi juu ya yesu familia hiyo mara tu hushindwa. Alihimidha watu kuwa na msingi imara na msingi huyo ni kujenga juu ya Yesu.

Apostle Linda Gobodo

MCHUNGAJI MUGISHA HENRY: Yeye aliongeya juu ya thamani za familia, kujenga juu ya maandiko matakatifu BIBLIA. Neno ambalo tunalisoma katika kitabu cha Nehemia 4:13-14.

MUGISHA Henry

Thamani gani tunazo zihitaji? Hapa nitasema mambo 2.
  1. Kuelewa vizuri kwamba familia yako ipo kwenye Meli, kama vile familia ya Noah ilikuwa Pamoja kwa Meli wakati wa gharika. Na Meli hiyo kwa leo ni kanisa la Bwana.

Hakika siku za leo Watoto wanaamka na mpango tofauti siku ya jumapili, wengine huwa wanauliza wala kuwakumbusha wazazi wao kuwapeleka kanisani. Na labda wazazi wanasema unajuwa nilikuwa na kazi nyingi kwa wiki hii, kumbe leo nitapumzika nitaomba wiki ijayo. Lakini kumbukeni kwamba biblia inasema ukumbuke siku ya sabato na uitakase. Kumbukeni ya kwamba Yobu alikuwa na wakati wa maombi ya Pamoja na ilipokuwa jioni yeye hua anasema labda Watoto wangu kwenye sherehe zao wamemukoseya Mungu na alikuwa akifanya maombi ya kuwatolea msamaha. Yobu 1:15

Mimi nimewazoweza Watoto wangu kuomba hata ingawa tupo kwa Gari nikiwapeleka shuleni, huwa nawaambia kuomba, na ninashukuru Mungu kwa sababu mtoto wangu kijana kuliko wote hu ahata anawakumbusha wenzake kuomba.
2. Mtume Linda amesema ya kwamba Mungu ni Mungu wa vizazi. Nataka niwaambiye haya: mtakapo ona Watoto wenu hutia viatu vya wazazi, musiwakaripiye wala kuwacheka kwa sababu, vinamanisha ya kwamba wanawaiga wazazi wao, matendo yale munayo waonyesha Watoto wenu nao pia watayaiga na kuyafanya.
ASKOFU Dr. GAHUNGU BUNINI: Alianza na kuwambia maneno ya mtaalamu alisema kwamba kila swali lilo mbele ya watu lazima lipate suluhisho. Aliongeya juu ya funguo saba zinazo wasaidia watu kuishi kwa Pamoja. Funguo nikitu mhimu sana, mara tu funguo ya chumba ikipoteya utakuta watu wamekosa amani.
  1. Historia ya kila mmoja kwenye ndoa: Zaburi 90:12, kila mara watu husahau mengi mema mwenziwe ameyafanya na kuhesabu kosa moja tu, zidi ya mema hayo. Baada ya kuangalia kosa hilo ebu rudi nyuma uyahesabu mengi mema na utajuwa ya kwamba yaliyo mufikiya yeye pia ni mwanadamu bali si Malaika, ataweza akakoseya.

  1. Kumbuka baraka zote mulizo zipata tangu muishi naye: Zaburi 126:1. Uhesabu baraka zote bila kuacha hata moja. Mara nyingi mjini Kigali watu wanaishi Pamoja kwa amani wakiwa maskini lakini wakitajirika wanachana. Ametowa mfano ya mke aliye wapokeya inchini amerika alimuuliza eti mbona naona una mali mengi kwa nini umeachana na mume wako? Naye akamjibu ya kwamba chanzo cha kuachana ni hizo mali.

  1. Mda murefu wa kuishi Pamoja isikuwe chanzo cha kuwamaliza nguvu na kuachana bali mda mrefu mkiishi Pamoja iwape nguvu ya kumuiga kila mumoja, na kupendana tujifunze kwa wengine. Mwanzo 40:23

  1. Kuhesabu vitendo mbalimbali: kuna vikwazo kadha wa kadha ambavyo tumevuka Pamoja kama vile njaa, magonjwa, umasikini…, Kutoka 15:1.

  1. Kukumbuka wale Mungu aliinua ili kuwasaidia kufika kwenye lengo lenu. Biblia inasema ya kwamba wawili wazidi mmoja, kwa sababu mmoja akianguka mwengine humushika mkono na kumuinua. Shida tunayo kwa sasa ni kwamba watu wa leo hakubali kuchangia Baraka. Ruth 1:15, Mwanzo 30:27.

  1. Kuomba maombi ya Pamoja: kufanya mambo kwa Pamoja ni baraka kubwa Zaidi. Matendo ya Mitume 10:2

  1. Kufunga milango ya Hasira na kufunguwa milango ya msamaha. Msamaha ndio funguo peke litaweza wasaida watu kuishi kwa Pamoja mda mrefu. Filemoni 1:17-19.

Dr. GAHUNGU BUNINI:

MASWALI NA MAJIBU
Ingawa wazazi wanafanya chochote wakiwezavyo, lakini kati ya Watoto kunaonekana mmoja ambaye ameshindikana, nani tumutuhumu? 
Jibu ni kwamba Watoto wetu ni wazuri, lakini wanahitaji mshahuri, tuwashahuri Watoto wetu bila kukoma.
Kama mke anpigwa fimbo mbele ya Watoto, na kuhibishwa kwa mda mrefu, je ni lazima kuendelea kuishi na huyo bwana wala kumuacha ndiyo sulihu nzuri, swali hili lilijibiwa Pamoja na linguine liulizavyo je kuporomosha mimba ni dhambi?
Jibu ni kwamba kila kitu kinyume ya neno la Mungu ni dhambi.
Wazazi walishuriwa kuendelea kuwasogeleya Watoto wao hasa Zaidi kwa miaka hiyo wanayoyiita ya ukaiidi. Kwa sababu kile ambacho Watoto wanahitaji kwa wazazi wao ni upendo. Na kuwaongoza kwa upole na upendo.

MTUME Dr. PAUL GITWAZA:  Alianza kuonyesha tofauti kati ya familia ya kwanza ambayo biblia inasema katika agano la kale na familia kama kanisa la Bwana katika agano Jipya. Yesu alijuwa vizuri kama familia ya kwanza katika kitabu cha mwanzo iliyo anzwa na Admu wa kwanza haikufaulu, basi yeye akaja kama Adamu wa mwisho na philosophia nyingine ya kuilinganisha familia na Kanisa kama tunavyo visoma katika baruwa ya mtume Paulo kwa wa Efeso.
Ametowa mfano wa mwanamke msherati, aliyekuwa mke wa mchungaji wa kanisa huko inchini DRC, na wakati tu alikuwa anajuwa ya kwamba mume wake ameenda safarini alikuwa huwaleta wakristo wa kanisa lake kulala Pamoja naye. Basi ikawa siku moja huyo muchungaji alitaka Kwenda kuhuzuria mkutano mahali pengine alipofika kwa kituo cha gari la moshi, akakuta tayari imekwisha ondoka na kumuacha. Ilibidi arudi nyumbani, alipofika akamkuta mke wake analala na bwana mwengine, akatoka akaenda dukani kununua mkate na maziwa na kuwapigia chai, na alipomaliza akawaita ili waje wale kwa sababu alijua wanachoka. Lakini hawakuweza kutoka chumbani kwa kuwaza ameandaa panga la kumkata, na alipona kwamba wamekataa Kutoka wachangiye, basi alimuita mkristo wake aje arudi nyumbani. Akaja akiinama kuhofia asikatwe na kumufungulia akaenda zake, akamtakia kila la heri. Alipofika chumbani alimuongelesha mke wake kama kawaida, lakini kwa haya nyingi sana hakujibu. Basi ilipokuwa mda wa usiku wamanane akasikiya mke wake akipiga kelele na alipoamka ili kumusaidia akaona Malaika akiwa na kisu ya makali sana akamwambiya ukitaka kumusaidia mke wako nitakuangamiza. Basi mume akalala na hayo yalitendeka mpaka karibu alfajiri. Na baada yah apo mke akaamuka na kumuomba mume wake huruma, na kumwambiya ya kwamba sitakwambiya yaliyo nipata bali yote nitayaneneya kanisani. Na asubuhi yake wakaenda kanisani akawaita wale wote walio lala naye karibu wanaume wote wa kanisa. Na kitendo hicho kimefufua uamusho kwa sehemu nyingi za inchi hiyo.
Alimaliza akiombeya familia za sasa ili Mungu apate kuwalinda na kuwasaidia, kwa kuwa ndoa za sasa unapo jaribu kuzishahuri hazikuelewi.

Apostle Dr. Paul M. Gitwaza

Posted in , ,

Recent

Archive

 2024
 2023
 July
Global Youth Arise: A Transformative Journey to a purposeful lifeGlobal Youth Arise: Building Families on a firm foundationGuide to preparing for the courtship processYouth Arise Day 2 Revival Service: Whom shall I send?Mkutano wa vijanaGlobal Youth Arise Day 2: Unveiling your divine callingApostle Gitwaza revealed seven primary callingsSpeech | Apostle Dr Paul Gitwaza | Africa Haguruka 2023 Ijambo rya Apostle Dr Paul Gitwaza | Africa Haguruka ku nshuro ya 24Africa Haguruka 2023 - Mountain of FamilyOpening Remarks by Archbishop MbandaApostle Dr Paul Gitwaza Unveils Africa's Rich History: Africa's Rich Legacy as a Reflection of God's Divine Plan for Humanity"Africa Haguruka Day 3 - Mountain of EducationIndangagaciro 10 zafasha Afurika gutera imbere | Africa Haguruka 2023 Embracing the Mentorship of God - A Call to Africa's RevivalAfrika Inuka 2023 | Siku ya 2 | Mlima wa FamiliaMulima wa Elimu: Njia Iletayo MageuziSALVATION IS NOT A BOREDOM: Spread the Gospel and embrace the world's diversity through art and entertainmentUmunsi wa 4 w'igiterane cya Afrika HagurukaShifting Foundations and Unveiling a New Destiny | AH24tume Linda Gobodo amtangaza yesu christ kuwa Mshauri mkuu zaid duniani hajapataUnlocking Business Potential | Africa Haguruka 2023Africa Haguruka 2023: Umusozi w'UbucuruziAFRICA ARISE 2023: Apostle Linda Gobodo Declares Jesus Christ as the Greatest Mentor the World Has Ever SeenUmwuka wera nk'umutoza wa AfrikaMkutano wa Uamusho: Simama kwenye msingi imara | Siku ya 4A Call for Transformation and MentorshipUmunsi wa 5 w’igiterane cy’Africa Haguruka | #AH24Umusozi w'idini | Afrika Haguruka 2023Empowering transformation through mentorship and the holy spirit at Mount Hermon, KigaliEjo hazaza ha buri kimera hagenwa n’ubwiza n’umwimerere bw’iyo mbuto | #AH24Empowering Transformation for God's GloryGod Will Bless African, A Blessing That Will Change the Way the Entire World Perceives the ContinentMwito wa mageuzi na ushahuriKumenya umutoza wa Afrika wifashishije ibyayihinyuje ndetse n'ibyiringiro byayoUnravelling the secret code of Africa's evolution A Journey of Challenges and HopeThe Distinguishing Traits of Church Leaders Mentored | Africa Haguruka 2023The Church in Africa Must Seize and Own the Stick of Command

Categories

Tags