Mulima wa Elimu: Njia Iletayo Mageuzi

KIINGILIO
Kwenye Siku yake ya tatu ya mkutano Afrika Haguruka, ilikuwa semiari juu ya “Mlima wa Elimu”. Aliye ongoza mkutano huo alikuwa Mchungaji Flory, Pamoja na Mtafsiri wake Vanessa, baada ya kuomba na kuabudu aliwaita wajumbe ambao walialikwa kuhutubia mkutano, kati yao kulikuwa Ndugu Ben Musuhuke, Ambassodor Dr. Charles Murigande na Dr. Philip Igbinijesu.

Mchungaji Flory

Ndugu BEN MUSUHUKE: Yeye alianza akihutubia waliokusanyika kwa kuwaonyesha tofauti iliyoko kati ya Elimu iliyo ya kweli ama inayostahili na Elimu ya ki Afrika. Alijaribu kuonyesha yale ambayo yanahitajika ili Elimu ieneye. Alisema kwamba elimu ambayo haifwate taratibu za biblia, elimu hiyo mara nyingi haifaulu., alionyesha yale yanayo faa ili elimu iwe na sura ya maguezi kwa bara lote la Afrika ni kwamba. Na aliongeza ya kwamba kutokuwa na umoja, kukosa vitabu vya muongozo (curriculum), kutokuwa na tabia nzuri hayo yote ni mojawapo ya vikwazo tunavyo kwa ajili ya kupata Elimu inayofaaa.
Bwana Musuhuke amesema ya kwamba tukiwa na vitabu vya muongozo vizuri vya kuanzia kwa Watoto wachanga, utafiti na pia kuingiza technologia mpya na kuwa na mshahuri mzuri kuanzia nyumbani hadi shuleni hayo yote ndiyo yatatusaidia kuweza kupata Elimu inayohitajika.

Ndugu Ben MUSUHUKE

Rev. Dr. PHILIP IGBINIJESU: Yeye alipo pewa nafasi ya kuongea, kwa masharti makubwa ya kiblia yanayo hitajika kuingizwa kwenye Elimu. Katika masharti hayo muna yale kama: Ujuzi wa kujua kutafuta suluhu, kuwaza mbali na kuvumbua vitu vipya, kuwa na uwezo wa kujisikiya kama unaweza, kuwageuza wanafunzi kuwa viongozi wa siku zijazo.
Amesoma maandiko katika kitabu kitakatifu cha Mungu kama: Mithali 19:2; Yohana 6:6; Mchungaji Igbinijesu alisema ya kwamba Kanisa limezoea kubaki nyuma kwa kila Jambo, hapa alitoa mfano ya kwamba kitu kimoja pekee kanisa liliongoza ni Imprimante. Bali nyuma kumekuja mabadiliko kadhaa wala kanisa halikuhusu, ametaja Radio, Runinga (TV), kukafuata technologia ya simu za mukononi, na baada kulikuja mitandao ya kijamii, leo sasa tunayo ingine maendeleo ya vitu kama pesa za hewani (crypto currency), akili yakutengenezewa (Artificial Intelligence), wala tena technojia mpya ya Chat GTP na kadhalika. Alimaliza akisema ingekuwa wakristo wamekuwa kwa mstari wa kwanza na kuongoza milima hiyo yote kama leo tunayo matokeo mazuri, lakini kwa sababu technolojia inaongozwa na watu wa dunia hii, mambo memgi tutakayo yakuta kwa mitandao ya kijamii yote itaonyesha watu wa dunia. 

Rev. Dr. PHILIP IGBINIJESU

AMBASSODOR Dr CHARLES MURIGANDE: Alianza na kutafsiria elimu ni nini?, na kuonyesha mafaa ya elimu kwa kila kiumbe. Na alisema ya kwamba elimu haipashwi kuyasahau umuhimu wa kuwa na msingi ndani ya masharti ya biblia, na msingi mkubwa kwa kila kitu ni Mungu. Alisema ya kwamba Yesu ndiye mwenyewe msingi kwa kila jambo. Na kway eye mataifa wote huokolewa.

Ambasador Dr. Charles MURIGANDE

MASWALI NA MAJIBU
Dr. Philip Igbinijesu alijibu swali ambalo liliuliza, kanisa litaweza husika namna gani ili kuhakikisha elimu inafuata msimamo ya kikristo? Na pia kujibu kwa technologia ya AI, kwa Watoto wa kizazi cha sasa? Alijibu ya kwamba ingekuwa heri kanisa kuja kwa mstari wa mbele katika kila sehemu na kujaribu kupaza sauti kwa mataifa tukishika fursa hiyo ya kuwatangazia mataifa Habari njema za Yesu Kristo, mbele ya matangazo mengine ya dunia.
BEN MUSUHUKE: Yeye alihimiza waliokusanyika ya kwamba elimu nzuri ni yenye kuanzia kwa Watoto wa umri mudogo na yenye kuanzia nyumbani, na yenye washahuri wazuri. Nawaza elimu hiyo inaweza badilisha taifa.
Dr. CHARLES MURIGANDE: Kwa sasa tunahitaji elimu ile ambayo si ya walimu, kuwapa yale walio nayo bali ni elimu ambao inasaidia wanafunzi kufanya utafiti na kugundua wenyewe. Na mwisho bishop Leonard alisema ya kwamba Watoto wetu wawe makini kwa kutumikisha technologia, akisema ya kwamba hata yale tunayaona kwamba ni mema tujuwe ya kwamba kuna vingine vinavyo jificha nyuma.
MTUME PAUL GITWAZA
Kwakufunga mkutano wa leo Mtume Paul alijubu swali ambalo alikuwa ameulizwa yakwamba yawazekana mtu ambaye hakusoma kuongoza kanisa? Kwa mfano wale ambao waanasema wameitwa na roho mtakatifu na kuwapa nguvu na ufunuo wakuliongoza kanisa.
Jibu alisema ya kwamba inewezekana lakini kwa sababu hakusoma atakuwa na mipaka labda ya lugha, ya kusoma na kuandika. Amesema mengi  kwa ajili ya mitume wa Yesu ambao wengi kati yao hawakusoma lakini walipata uwezo kupitia nguvu za roho mtakatifu, kuisamba injili na kuineza dunia nzima.
Amerudi pia kwa technologia hii ambao inasemekana sana kwa siku hizi ya AI. Amesema kwamba mtu ambaye amegundua technogia hiyo alikuwa mutu amesoma mambo ya kisakologia (maumbile ya Mwanadamu). Baada yah apo alirudi nyuma na kuwanza kuwa ginsi ataweza gueza mafikiri hayo ya mwanadamu na kuitia ndani ya computer. Alipomaliza kuona ana kitu kipya, alianza kutafuta mashirika ambayo itamuunga mkono, nah apo alipata kushirikiana na kiongozi wa Microsoft. Walipoanza kutumika naye akaona technogia yake inasonga mbele alianza ogpa na kusema tuyaweke sheria ambazo zitazuia watu Kwenda mbali ya ujuzi wao.
Mtume Paul alifunga mkutano kwa maombi. Bwana awabariki nyote.

Apostle Dr. Paul Gitwaza

Posted in ,

Recent

Archive

 2024
 2023
 July
Global Youth Arise: A Transformative Journey to a purposeful lifeGlobal Youth Arise: Building Families on a firm foundationGuide to preparing for the courtship processYouth Arise Day 2 Revival Service: Whom shall I send?Mkutano wa vijanaGlobal Youth Arise Day 2: Unveiling your divine callingApostle Gitwaza revealed seven primary callingsSpeech | Apostle Dr Paul Gitwaza | Africa Haguruka 2023 Ijambo rya Apostle Dr Paul Gitwaza | Africa Haguruka ku nshuro ya 24Africa Haguruka 2023 - Mountain of FamilyOpening Remarks by Archbishop MbandaApostle Dr Paul Gitwaza Unveils Africa's Rich History: Africa's Rich Legacy as a Reflection of God's Divine Plan for Humanity"Africa Haguruka Day 3 - Mountain of EducationIndangagaciro 10 zafasha Afurika gutera imbere | Africa Haguruka 2023 Embracing the Mentorship of God - A Call to Africa's RevivalAfrika Inuka 2023 | Siku ya 2 | Mlima wa FamiliaMulima wa Elimu: Njia Iletayo MageuziSALVATION IS NOT A BOREDOM: Spread the Gospel and embrace the world's diversity through art and entertainmentUmunsi wa 4 w'igiterane cya Afrika HagurukaShifting Foundations and Unveiling a New Destiny | AH24tume Linda Gobodo amtangaza yesu christ kuwa Mshauri mkuu zaid duniani hajapataUnlocking Business Potential | Africa Haguruka 2023Africa Haguruka 2023: Umusozi w'UbucuruziAFRICA ARISE 2023: Apostle Linda Gobodo Declares Jesus Christ as the Greatest Mentor the World Has Ever SeenUmwuka wera nk'umutoza wa AfrikaMkutano wa Uamusho: Simama kwenye msingi imara | Siku ya 4A Call for Transformation and MentorshipUmunsi wa 5 w’igiterane cy’Africa Haguruka | #AH24Umusozi w'idini | Afrika Haguruka 2023Empowering transformation through mentorship and the holy spirit at Mount Hermon, KigaliEjo hazaza ha buri kimera hagenwa n’ubwiza n’umwimerere bw’iyo mbuto | #AH24Empowering Transformation for God's GloryGod Will Bless African, A Blessing That Will Change the Way the Entire World Perceives the ContinentMwito wa mageuzi na ushahuriKumenya umutoza wa Afrika wifashishije ibyayihinyuje ndetse n'ibyiringiro byayoUnravelling the secret code of Africa's evolution A Journey of Challenges and HopeThe Distinguishing Traits of Church Leaders Mentored | Africa Haguruka 2023The Church in Africa Must Seize and Own the Stick of Command

Categories

Tags